Monday 26 December 2022

MKUTANO WA MWISHO WA MWAKA WA NJENJE FAN CLUB WAFANA

 WAPENZI wa Kilimanjaro Band katika kundi lao linalojulikana kama Njenje Fan Club wakiwa na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo, leo walikuwa na mkutano wao wa kufunga mwaka 2022. Kilimanjaro Band inatarajiwa kuanza kufanya maonyesho ya kawaida ya kila wiki mapema mwanzoni mwa 2023. Bendi imo katika matayarisho ya  kusherehekea miaka 50 toka kuanzishwa kwa bendi hiyo.












Geophrey Kumburu - mpiga keyboards Kilimanjaro Band








Monday 26 September 2022

KILIMANJARO BAND WAWASHA MOTO DODOMA, IT WAS GREAT

 

Nyota Abdallah

JUMAMOSI tarehe 24 Septemba 2022 ilikuwa siku ambayo kwa mara ya kwanza bendi ya Kilimanjaro Band ilifanya onyesho katika uwanja wa maegesho ya magari wa Capital City Mall. Muziki ulianza rasmi saa 4 usiku kwa muziki wa taratibu na ilipofika saa tano Njenje wakaanza kwa kupiga wimbo maarufu wa Njenje. Kisha kukawa na mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki kama ilivyo kawaida ya bendi hii. Vijana wadogo wapya ambao wamechukuliwa kuendeleza bendi hii hakika waliweza kuzikonga nyoyo za washabiki wakiokuwepo katika onyesho hilo.

Martha, muimbaji mpya wa Kilimanjaro Band

Abou Mwinychumu

Mkongwe Mohamed 'Moddy' Mrisho

John kitime


Monday 29 August 2022

WANAMUZIKI WATATU WAJIUNGA NA KILIMANJARO BAND

 

KUMBURU

Baada ya kifo ya Waziri Ally, kiongozi na mpiga kinanda wa Kilimanjaro Band, bendi ilipata pigo kubwa ambalo limechukua muda mrefu kupata ahueni.
 Ili kuendeleza bendi hii kongwe  iliyoanza mwanzoni mwa miaka ya 70 kule Tanga, wanamuziki wapya watatu wamejiunga na kuanza mazoezi makali na bendi hii.
 Kwanza kabisa kuna mkongwe Geophrey Kumburu, huyu ni mpiga kinanda wa miaka mingi ambaye kati ya bendi alizopitia ni Kilimanjaro Connection, MK Group, Vijana Jazz band,Wahenga band, JFK Band na kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi peke yake ikiwemo kuendesha  na studio ya kurekodi muziki. Na kufundisha muziki. Geophrey pia ni muimbaji na ndie amechukua jukumu la kupiga kinanda katika bendi hii kongwe. Pia kuna vijana wadogo wawili ambao ni waimbaji, Martha na Feisal ambao ni wazi uwezo wao uko juu na utaleta nmchango mkubwa katika Kilimanjaro band.

Thursday 25 August 2022

TANZIA MZEE ALLY SEIF, BABA YAKE WAZIRI ALLY AFARIKI TANGA

 

MZEE ALLY SEIF

KWA MASIKITIKO MAKUBWA KILIMANJARO BAND INGEPENDA KUWATANGAZIA KIFO CHA MZEE ALLY SEIF, BABA YAKE ALIYEKUWA MPIGA KINANDA WA KILIMANJARO BAND, MAREHEMU WAZIRI ALLY.

KIFO KIMETOKEA TANGA NA MAZISHI YATAKUWA KESHO JUMAMOSI SAA 7 HUKOHUKO TANGA.

MUNGU AMLAZE PEMA MZEE ALLY SEIF

Tuesday 16 August 2022

KILIMANJARO BAND NJENJE YAANZA KUJIFUA KURUDI ULINGONI

 


NI mwaka mmoja toka mpiga kinanda na kiongozi wa Kilimanjaro Band Waziri Ally Seif alipofariki, bendi ya Kilimanjaro, wana Njenje walikuwa kimya kwa kipindi karibu chote, sasa bendi hiyo imo katika mazoezi makali na inategemea kuanza onyesho lake la kwanza katika jiji la Dodoma kabla ya mwisho wa mwezi huu. Usikose kutembelea humu kupata taarifa za ratiba ya bendi hii.



ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA